News Flash

On his last day in Tanzania, President Clinton became one of 360, 000 visitors annually to explore the World Famous Ngorongoro Crater. Often called "Africa’s Eden" and the "8th Natural Wonder of the World," this collapsed volcano (a “caldera”) is located in the Ngorongoro Conservation Area . This is a natural sanctuary for thousands of birds, insects and animals such as lions, zebra, black rhino and wildebeest, all free to wander.
 
Home arrow Tanzanians arrow Announcements arrow KUSITISHA PASIPOTI ZA ZAMANI
KUSITISHA PASIPOTI ZA ZAMANI Print E-mail
KUSITISHA KUPOKEA MAOMBI YA PASIPOTI ZA ZAMANI (MASHINE READABLE PASSPORT-MRP)

Ubalozi umepokea barua kutoka Idara ya Uhamiaji ikiarifu kuwa kuanzia tarehe 30 Aprili 2019 maombi ya pasipoti za zamani (MRP) yamesitishwa kupokelewa kutoka kwa Watanzania waishio nje (Diaspora), na badala yake wanaohitaji waanze kujaza maombi ya pasipoti za Kielektroniki (ELECTRONIC PASSPORTS).  wakati wakisubiri kufungwa kwa mitambo ya mfumo huo Ubalozini.

Ubalozi pia unapenda kuwakumbusha kuwa mwisho wa matumizi ya pasipoti za zamani za MRP ni mwishoni mwa mwezi Januari 2020. Hata hivyo, hatujafahamu tarehe kamili ya kufungiwa mitambo hiyo ingawaje kwa mujibu wa maelezo ya Uhamiaji ni kwamba Ubalozi wetu utafungiwa mwishoni mwa mwezi Juni au mwanzoni mwa Julai 2019.

Ubalozi unapenda kuwashauri wale wenye mahitaji ya haraka na wale watakaobahatika kwenda nchini Tanzania watumie muda huo wa likizo kuombea nchini pasipoti hiyo mpya.

Tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu na tutaendelea kupeana taarifa pindi tutakapofungiwa mitambo husika.
 
UBALOZI WA TANZANIA SWEDEN
+46 8 7322430 
   
Last Updated ( Tuesday, 14 May 2019 )
 
< Prev   Next >
© 2019 Embassy of The United Republic of Tanzania - Stockholm, Sweden

Comments for Webmaster
.