Kwa Watanzania waishio Ukraini

Ukurasa huu ni maalum kwa ajili ya taarifa muhimu kuhusiana na hali ya usalama nchini Ukraini kwa Watanzania waishio humo na mipaka yake. Pamoja na mifumo mingine ya taarifa, Ubalozi pia utatumia ukurasa huu kuweka taarifa rasmi kwa uma kadiri zitakavyo kuwa zikipatikana.
 • Taarifa – Wanafunzi Waliopo Mji Wa Sumy Ukraini
  Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Stockholm Sweden pamoja na Ubalozi wa Jamnuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Moscow Urusi, tunapenda kuwataarifu wanafunzi wa kitanzania walioko kwenye mji wa Sumy nchini Ukraini kwamba kupitia njia za kidiplomasia , Serikali ya Urusi imeridhia wanafunzi walioko Sumy State University kutoka nchini Ukraini kwa kupitia mpaka […]
 • Uhakiki – Taarifa Za Kimtandao Na Vyanzo Vyake
  NI MUHIMU KUJIRIDHISHA NA TAARIFA KABLA YA KUZITUMIA AU KUZISAMBAZA Katika kipindi hiki cha hali ya hatari inayoendelea nchini Ukraini ni muhimu kwa Watanzania walio katika eneo na mipaka ya nchi hiyo kuwa makini. Epuka kufanya malipo ya fedha kwa ahadi ya huduma za uokoaji au usafiri. Epuka kutoa taarifa au maelezo binafsi ya aina […]
 • Dharura Ukraini – Taarifa
  TAARIFA KWA WATANZANIA Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Berlin Ujerumani, pamoja na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Stockholm Uswidi, tunapenda kuwataarifu watanzania wote wanaotokea Ukraini kuelekea katika mipaka ya magharibi ya nchi hiyo kama ifuatavyo: (1) Tunaendelea kuratibu kwa karibu taarifa za Watanzania wanaotoka Ukraini kuelekea nchi za Poland, […]
 • Watanzania Waishio Nchini Ukraine
  Kufuatia hali tete ya kiusalama nchini Ukraine, Ubalozi unawashauri watanzania wote waliopo nchini humo hivi sasa kuwa watulivu na kuzingatia miongozo inayotolewa na serikali ya Ukraine. Kwa upande wa wanafunzi kutoka Tanzania wanaosoma nchini Ukraine, Ubalozi unawaomba kuendelea kuzingatia miongozo inayotolewa na vyuo wanavyo soma. Aidha, Ubalozi unaendelea kupokea taarifa za watanzania wote waliopo nchini […]