Loading Events
This event has passed.

Ubalozi wa Tanzania ulipokea wageni ikiwa ni Timu ya Wataalamu toka Walaka wa Majengo Tanzania tangu tarehe 29 May 2019 hadi tarehe 8 Juni 2019. Timu hii iliyotumwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilikuja kuendelea na mkakati wenye nia ya kujenga na kurekebisha majengo yanayomilikiwa na Serikali ya Tanzania na yanayotumiwa na Ubalozi wa Tanzania hapa Sweden.

Katika Picha ya pamoja na Mh. Balozi Slaa ni Bw. Edward Ngowi (Mkuu wa Msafara), Bi Matapuli Juma, Bw. Daniel Mwakasungula Bw. Mohamed Mohamed na Wafanyakazi wa Ubalozi Bw. Matiku Kimenya, Bi Prosister Swai, Bi Joyce Malipula na Bi Agnes Mwaiselage