The Government of the United Republic of Tanzania has reviewed the cost of the COVID-19 Test for travelers and decided to reduce the cost from 100USD to 50USD for RT PCR Test. The Government has also reduced the cost of Antigen RAPID TEST to 10USD for air travelers. Also, the cost for Antigen RAPID TEST has been removed altogether for travelers using other borders. These changes will be effective from 16th August 2021.
______________
Baada ya Mapitio pamoja na uchambuzi wa gharama za upimaji wa ugonjwa wa UVIKO-19, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepunguza gharama za upimaji wa ugonjwa huo kutoka dola 100 za Marekani kwenda dola 50 kwa kipimo cha RT PCR.
Pia serikali imeondoa gharama za kipimo cha Antigen RAPID TEST mipakani, na kutoza gharama ya dola 10 za Marekani kwa kipimo cha Antigen RAPID TEST kwa wasafiri wa viwanja vya ndege. Mabadiliko haya yanaanza tarehe 16 Agosti 2021.
Taarifa kamili hapa chini…
TAARIFA KWA UMMA GHARAMA 11 AGOSTI 2021