Uhakiki – Taarifa Za Kimtandao Na Vyanzo Vyake

NI MUHIMU KUJIRIDHISHA NA TAARIFA KABLA YA KUZITUMIA AU KUZISAMBAZA

Katika kipindi hiki cha hali ya hatari inayoendelea nchini Ukraini ni muhimu kwa Watanzania walio katika eneo na mipaka ya nchi hiyo kuwa makini.

  1. Epuka kufanya malipo ya fedha kwa ahadi ya huduma za uokoaji au usafiri.
  2. Epuka kutoa taarifa au maelezo binafsi ya aina yoyote kwa taasisi au mtu yeyote kabla ya kuhakiki urasmi wa taasisi husika.
  3. Ni muhimu kuhakiki taarifa zozote za msaada (bila kujali chanzo cha taarifa husika) kabla ya kuzitumia.
  4. Ni vema kuwasiliana na mamlaka rasmi za kiserikali kama Ofisi za Balozi zetu, Taasisi rasmi za kiserikali, au mamlaka za nchi uliyopo. 4.a. Mawasiliano ya Ubalozi wa Tanzania Uswidi (+46720494576) 4.b. Mawasiliano ya Ubalozi wa Tanzania Ujerumani(+4915215117558)
  5. Ni muhimu kufuatilia kwa ukaribu vyanzo rasmi vya taarifa, ikiwemo tovuti za Balozi zetu za Uswidi na Ujerumani.

ANGALIZO Kumbuka kwamba kusambaza taarifa zisizo sahihi (hasa katika hali ya hatari inayoendelea sasa) ni kinyume cha sheria za mataifa, na unaweza kushitakiwa kwa makosa ya jinai.

TAARIFA RASMI TOKA UBALOZI

Ubalozi umefungua ukurasa maalum kwa ajili ya taarifa zinazohusiana na Ukraini

Share This Post

More To Explore

Vice President Visit to Stockholm

The Vice-President Of The United Republic Of Tanzania, Dr. Philip Isdor Mpango Attends Stockholm+50′ Conference Read more…

Fursa Ya Uwekezaji Wa Nyumba Kwa Diaspora

Ubalozi unapenda kuwajulisha kuhusu fursa ya uwekezaji wa nyumba chini ya mradi uitwao Hamidu City Park uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Mradi huo unaomilikiwa na Bw. Hamidu Hemed Mvungi, una eneo lenye ukubwa wa ekari 140 ambalo lina nyumba 120 hivi sasa, zinazouzwa kwa gharama ya kuanzia Dola za Kimarekani 57,000 hadi 140,000. Kwa

Karibu Tanzania

The land of Kilimanjaro