Ujumbe Kutoka Kwa Balozi Mh. DKT Willibrod Slaa

Ndugu zangu Watanzania,
Napenda kuwasalimia popote mlipo katika nchi zetu za Uwakilishi, Sweden, Denmark, Iceland, Norway, Finland, Estonia, Latvia, Lithuania na Ukraine. Naamini nyote mko salama mkiendelea na majukumu yenu ya kila Siku. Naomba kutumia fursa hii kuwaletea ujumbe huu muhimu sana.

 1. Tarehe 10 Septemba, 2019 tuliwataarifu kupitia ukurasa wetu wa fb, Whatsapp groups zenu mbalimbali, kupitia Viongozi wenu wa Vyama vya Watanzania na kila aina ya mawasiliano iliyowezekana kuwa Ubalozi wetu umekwisha kufungiwa Mashine za Electronic Passports(E-Passport) na Electronic Visa( E- Visa).
 2. Aidha Mtakumbuka kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikwisha kutangaza kuwa Passport za sasa zitakoma kutumika Mwezi Januari 2020. Baada ya muda huu, hutaweza kupita viwanja vyote duniani kwa kuwa viwanja hivyo na vituo vyote vya mipakani havitaruhusu upite kwa kutumia Passpoti ya sasa ya Tanzania
 3. Hivyo hii ni fursa ya pekee kujipatia Passpoti yako mpya.
 4. Maelekezo kamili kuhusu utaratibu wa kupata Paspoti mpya uko kwenye Mtandao. Yaani unatakiwa uingie kwenye Mtandao www.immigration.go.tz, ingia sehemu ya e-Service ambako utakuta Fomu ya Maombi ya Pasipoti. Mfumo wenyewe utakuongoza hatua zote zinazofuata. Aidha Ubalozi pia umetoa maelekezo hatua kwa hatua.
 5. Zingatia
  1. Hakuna maombi yanayopokelewa Ubalozini. Lazima ujaze Fomu hatua kwa hatua, na ukiisha kamilisha hatua ya kwanza yaani baada ya kulipa $ 15 na kupata risiti upige simu ubalozini ili upewe maelekezo ya Hatua ya pili. Baada ya kukamilisha hatua ya kulipia $75 utapewa Miadi ya kufika Ofisini kwa hatua zaidi. Katika hatua hakuna kumtuma mtu. Wewe mwenyewe unatakiwa kufika ubalozini kwa muda na siku utakayokuwa umepewa kwa ajili ya kupiga Biometric Photo, na kuweka saini yako mambo ambayo yanakuhitaji wewe mwenyewe hakuna mwakilishi.
  2. Taratibu nyingine utaelekezwa na Afisa wa Ubalozi anayehusika na masuala ya Pasipoti.

TAHADHARI.

 1. Kumbuka tuna muda mfupi sana umebaki kufikia Januari 2020. Naomba kila mmoja azingatie kuwa huo ndio muda wa mwisho kama ulivyotangazwa na Serikali. Usibahatishe vinginevyo ukipata haki yako hiyo hatutakuwa na namna ya kukusaidia.
 2. Tujitokeze sasa, ili tusiwe na msururu ambao tutashindwa kuuhimili kwa kila mmoja kungojea dakika ya mwisho
 3. Inawezekana wako watakaokuwa na tatizo la kuingia kwenye mtandao au mfumo nilioelekeza hapo juu. Ninaomba kila mmoja ajitahidi kupata msaada kutoka kwa mtoto, ndugu au jamaa na au viongozi wenu wa mahalia. Hii ni kwa sababu kila kitu kinatakiwa kufanyika kwenye mtandao isipokuwa yale mambo mahususi yatakayohitaji mtu kufika ubalozini.
 4. Kwa yale ambayo mtu atahitajika kufika ubalozini ni lazima mtu afike ubalozini. Tofauti na siku za nyuma ambapo Afisa ubalozi aliweza kuwatembelea kwenye maeneo yenu mfumo wa sasa hauwezeshi kusafiri na mitambo ambayo imeunganishwa mmoja kwa mmoja na Mfumo wa Immigration. Isitoshe mitambo husika ni mikubwa na mizito ambayo haiwezekani kuzunguka nayo.

Narudia kutoa Wito kwamba kila mmoja achukue hatua za haraka kujaza Fomu Mtandaoni ili kazi ianze mara mmoja,
Tunawatakia ufanisi wa haraka ili kukamilishi zoezi hili muhimu sana kwa manufaa yenu wenyewe

Kwa maelezo zaidi kuhusu Pasipoti, tafadhali tembelea ukurasa wa pasipoti

Share This Post

More To Explore

Vice President Visit to Stockholm

The Vice-President Of The United Republic Of Tanzania, Dr. Philip Isdor Mpango Attends Stockholm+50′ Conference Read more…

Fursa Ya Uwekezaji Wa Nyumba Kwa Diaspora

Ubalozi unapenda kuwajulisha kuhusu fursa ya uwekezaji wa nyumba chini ya mradi uitwao Hamidu City Park uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Mradi huo unaomilikiwa na Bw. Hamidu Hemed Mvungi, una eneo lenye ukubwa wa ekari 140 ambalo lina nyumba 120 hivi sasa, zinazouzwa kwa gharama ya kuanzia Dola za Kimarekani 57,000 hadi 140,000. Kwa

Karibu Tanzania

The land of Kilimanjaro