Watanzania Waishio Nchini Ukraine

Kufuatia hali tete ya kiusalama nchini Ukraine, Ubalozi unawashauri watanzania wote waliopo nchini humo hivi sasa kuwa watulivu na kuzingatia miongozo inayotolewa na serikali ya Ukraine.

Kwa upande wa wanafunzi kutoka Tanzania wanaosoma nchini Ukraine, Ubalozi unawaomba kuendelea kuzingatia miongozo inayotolewa na vyuo wanavyo soma.

Aidha, Ubalozi unaendelea kupokea taarifa za watanzania wote waliopo nchini Ukraine. Kwa wale ambao bado hawajawakilisha taarifa zao Ubalozini, wanaombwa kuwasilisha taarifa hizo ikiwemo Jina kamili, namba ya hati ya kusafiria, mji pamoja na namba ya simu. Taarifa hizo zitumwe kupitia barua pepe consular@tanemb.se

Barua rasmi ya maelezo haya toka ubalozini imeambatanishwa hapa chini.

USHAURI KWA WATANZANIA NCHINI UKRAINE

Share This Post

More To Explore

Vice President Visit to Stockholm

The Vice-President Of The United Republic Of Tanzania, Dr. Philip Isdor Mpango Attends Stockholm+50′ Conference Read more…

Fursa Ya Uwekezaji Wa Nyumba Kwa Diaspora

Ubalozi unapenda kuwajulisha kuhusu fursa ya uwekezaji wa nyumba chini ya mradi uitwao Hamidu City Park uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Mradi huo unaomilikiwa na Bw. Hamidu Hemed Mvungi, una eneo lenye ukubwa wa ekari 140 ambalo lina nyumba 120 hivi sasa, zinazouzwa kwa gharama ya kuanzia Dola za Kimarekani 57,000 hadi 140,000. Kwa

Karibu Tanzania

The land of Kilimanjaro