Ubalozi wa Tanzania Uswidi (Sweden) unaiwakilisha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi zifuatazo:
  • Nchi za Nordic ambazo ni Denmaki, Ufini, Isilandi, Norwey na Uswidi.
  • Nchi za Baltic ambazo ni Estonia, Latvia na Lithuania na Ukraine
Kwa hiyo, Ubalozi wa Tanzania Uswidi unatoa huduma za kiraia na nyinginezo kwa Watanzania na Diaspora wa Kitanzania wote waishio katika nchi zilizotajwa hapo juu. Ubalozi hutoa taarifa, hutoa huduma zilizoidhinishwa au hupokea maombi na kuyawasilisha nyumbani kama;
  1. Pasipoti na Hati za Kusafiria za Dharura.
  2. Kuukana Uraia
  3. Kuthibitisha hati mbalimbali
  4. Vyeti vya kutokuwa na  kipingamizi cha ndoa
  5. Hati za Tabia Njema nk.

Kujiandikisha na Takwimu za Diaspora wa Tanzania

Ubalozi umeanza kukusanya Takwimu za Diaspora katika eneo la uwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania uliopo Sweden. Diaspora wanatakiwa kujiandikisha kwa kupakua FOMU HAPA. Baada ya kujaza itume fomu hii Ubalozi kwa email: mailbox@tanemb.se Katika mwaka 2017/2018, takwimu zilizopatikana toka Idara za Takwimu katika nchi 6 kati ya 9 za uwakilishi wetu ni kama ifuatavyo: Idadi ya Watanzania ni 3282, na idadi ya wale waliochukua uraia wa nchi wanazoishi ni 2103. Kwa hiyo jumla ya wanadiaspora katika eneo la uwakilishi wa ubalozi ni 5385. Karibuni nyumbani!