Kwa wale wanaotakiwa kuwa na Hati ya Polisi ya Tabia Njema (Police Clearance Certifiate) toka Tanzania hatua zifuatazo zinatakiwa kufuatwa.

Mwombaji atatakiwa kwenda katika kituo cha Polisi kilichoko karibu naye ili achukuliwe alama za vidole (Certified Fingerprints). Kisha;
Andika barua ya maombi kupatiwa hati hii ya tabia njema.
Ambatanisha USD 25 kama malipo ya huduma ya kutayarisha hati pale CID Dar es Salaam
Ambatanisha nakala ya hati yako ya kusafiria (passport) ikionyesha jina lako sehemu iliyotolewa na tarehe itapoisha muda wake.
Ambatanisha karatasi halali zenye alama za vidole – zikiwa na jina, muhuri na sahihi ya afisa aliyechukua
Vitu hivi vyote vitume moja kwa moja kwa

Officer In charge
Forensic Bureau
Criminal Investigation Department Headquarters
P.O. Box 9094
DAR ES SALAAM

Simu: +255 22 211006, 2118637, au +255 754 827940.
Fax Na. +255 22 2112174

Matokeo ya uchunguzi wa taarifa za masuala ya makosa ya jinai (criminal record) hutolewa siku saba baada ya kupokea malipo na kuituma hati hiyo ya tabia njema kwa mwombaji.
*Ikiwa kuna matatizo juu ya ombi hili mwombaji anakaribishwa kuwasiliana na Ubalozi.