Ubalozi wa Tanzania, Sweden hautoi Vyeti vya Kuukana Uraia wa Tanzania bali inapokea tu maombi na kuyawasilisha Idara ya Uhamiaji, Wizara ya Mambo ya Ndani Tanzania. Hatua za maombi haya yanachukua si chini ya miezi mitatu kabla Cheti cha Kuukana Uraia kutolewa. Cheti kikitolewa kinatumwa Ubalozini na Ubalozi kukituma katika anuani sahihi ya mwombaji.

Mwombaji anatakiwa kujaza fomu mbili za maombi ya kuukana uraia (Pakua fomu hapa). Fomu hii inatakiwa ijazwe mbele ya Afisa anayeruhusiwa kupokea viapo. Huyu anaweza kuwa ni Afisa aliyeteuliwa na Wizara ya Sheria, Wakili, Hakimu au yeyote anayeruhusiwa kwa kutokana na Cheo au wadhifa wake.

Malipo ya huduma hii ni SEK. 1100 (elfu moja mia moja) ikiwa ni pamoja na gharama za posta. Ada ilipwe katika akaunti ya Ubalozi Post Giro Account: Anuani ni NDEASESS na International Bank Account Number (IBAN): SE2895000099604210374718. Risiti ya malipo iambatanishwe katika fomu za maombi.

Mahitaji mengine ni picha 3 za pasipoti, Pasipoti ya Tanzania (ili irudishwe Wizarani), barua aliyopewa ya kukubaliwa Uraia mpya (iwe kwa/imetafsiriwa kwa lugha ya kiingereza).